Page 45 - Historiayatznamaadili
P. 45
Baadhi ya jamii mpaka sasa bado zinaishi katika nyumba hizo.
Tofauti ya nyumba za asili na za kisasa, ni kuwa nyumba za
asili huwa na hewa safi na hazihifadhi joto kama ilivyo kwa
nyumba za kisasa. Aidha, ni rahisi kuzijenga na hazina gharama
FOR ONLINE READING ONLY
kubwa katika ujenzi. Tofauti za makazi kwa sasa zimetokana na
mwingiliano wa jamii. Hivyo, jamii zetu kuiga muundo wa ujenzi
wa makazi ya sasa.
Kazi ya kufanya namba 12
Tembelea eneo la karibu lenye makazi ya nyumba za
asili kisha:
1. Andika aina ya nyumba hizo na malighafi zilizotumika
katika ujenzi.
2. Chora picha ya nyumba ya msonge, banda na
tembe.
3. Andika mambo ya kujivunia kutokana na nyumba
za asili.
4. Andika mambo ya kujifunza kuhusu makazi ya asili.
Maendeleo ya jamii katika afya kabla ya ukoloni
Afya ni hali ya kuwa mkamilifu kimwili na kiakili. Kwa maana
nyingine, ni hali ya kutokuwapo kwa maradhi katika mwili wa
binadamu au kuugua. Jamii yenye afya inaweza kushiriki katika
shughuli za maendeleo binafsi, jamii na Taifa kwa jumla. Afya
bora husaidia kuleta maisha bora na kupunguza umaskini.
Kazi ya kufanya namba 13
Waulize wazazi au walezi kuhusu mambo
yaliyozingatiwa katika afya ya jamii yako hapo kale.
38
06/11/2024 11:29:48
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 38
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 38 06/11/2024 11:29:48