Page 38 - Historiayatznamaadili
P. 38
maeneo ya karibu na vyanzo vya maji ili kupata maji na samaki.
Pia, zilijenga kandokando ya milima ili kufanya shughuli za kilimo
na kukwepa mafuriko. Aidha, jamii za kale ziliepuka ujenzi katika
maeneo yenye wanyama wakali, yenye magonjwa, tetemeko la
FOR ONLINE READING ONLY
ardhi, mafuriko na vimbunga.
Aina za makazi kabla ya ukoloni
Jamii za kale zilikuwa na makazi ya aina mbalimbali. Aidha,
tofauti za ujenzi wa makazi hayo, ziliakisi malighafi za ujenzi
zilizopatikana katika mazingira ya jamii inayohusika. Mfano,
ujenzi ulifuata uwepo wa nyasi, mianzi, matete, miti mirefu
na mifupi, udongo na makuti. Pia, ujenzi wa nyumba hizo,
ulitegemea utamaduni wa jamii na ukubwa wa familia, kama
vile idadi ya watoto na wake katika familia. Mfano, jamii za
Wangoni na Wanyakyusa zilijenga nyumba kubwa na ndogo eneo
moja. Nyumba kubwa ilitumika kwa ajili ya wazazi na watoto
wadogo na ile ndogo kwa ajili ya vijana wa kiume. Wahehe
walijenga nyumba kubwa iliyokuwa na vyumba vingi kwa sababu
familia ziliishi pamoja. Wamasai walijenga nyumba kama boma
kulingana na idadi ya wake na watoto. Wachaga, Wahaya,
Wanyambo na Wasukuma walijenga nyumba mbili katika eneo
lao. Nyumba moja ilikuwa kwa ajili ya kulala watu na nyumba
nyingine kwa ajili ya kulala mifugo, kupikia na kuhifadhia mazao.
Baadhi ya jamii zilijenga nyumba moja, ambamo walitenga eneo
la kukaa watu na kulaza wanyama.
Kazi ya kufanya namba 9
Andika mambo uliyojifunza kuhusu ujenzi wa makazi
ya jamii kabla ya ukoloni ukilinganisha na ya sasa.
Muundo wa ujenzi wa makazi ya jamii za Kitanzania ulikuwa wa
aina tatu ambazo ni msonge, tembe na banda.
31
06/11/2024 11:29:41
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 31
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 31 06/11/2024 11:29:41