Page 33 - Historiayatznamaadili
P. 33
mzazi alikuwa mwalimu wa kwanza wa mtoto. Watu walijifunza
wakati wote katika mazingira yanayowazunguka ili kuwawezesha
kuyakabili mazingira yao. Hivyo, jamii za wakulima zilijifunza
kilimo, jamii za wavuvi zilijifunza uvuvi. Vivyo hivyo, jamii za
FOR ONLINE READING ONLY
wahunzi na wafugaji. Vijana walifunzwa pia majira ya mwaka;
kiangazi na masika. Watu walifundishwa kazi zilizofanywa katika
majira haya. Kimsingi, elimu kabla ya wakoloni ilifundisha watu
kujitegemea na kuyakabili mazingira yao.
Pia, vijana hasa wa kiume, walipofikia umri fulani walipewa
mafunzo ya ulinzi ili kulinda jamii zao. Vijana walifundishwa
kutengeneza silaha; kama vile pinde, mishale, mikuki na sime.
Aidha, kila mwanajamii aliandaliwa vizuri na alikuwa tayari
kulinda jamii yake. Kielelezo namba 2, kinaonesha vijana wakiwa
na silaha za asili za ulinzi.
Kielelezo namba 2: Vijana wakiwa na silaha za asili za ulinzi
26
06/11/2024 11:29:38
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 26 06/11/2024 11:29:38