Page 32 - Historiayatznamaadili
P. 32
Kazi ya kufanya namba 4
Soma matini mbalimbali kuhusu maana ya neno
ukoloni.
FOR ONLINE READING ONLY
Nchi yetu kwa nyakati tofauti, imetawaliwa na wageni kutoka
nchi za Ulaya. Mfano wa wageni hao ni kutoka katika nchi
za Ujerumani na Uingereza. Wageni hao walipokuja nchini
waliondoa utawala na mamlaka zilizokuwapo katika jamii zetu,
kisha kututawala kiuchumi, kisiasa na kijamii. Huo ukawa ndio
mwanzo wa utawala wa kikoloni nchini.
Kazi ya kufanya namba 5
Waulize wazazi au walezi kuhusu maendeleo ya jamii
yaliyokuwapo katika jamii yenu kabla ya ukoloni.
Maendeleo ya jamii katika elimu kabla ya ukoloni
Jamii zetu zilikuwa na maendeleo katika elimu, ingawa mfumo
wa elimu uliokuwapo, ulikuwa tofauti na huu tulionao sasa. Watu
hawakwenda shule na kuingia darasani kusoma, kuandika na
kuhesabu kama ilivyo sasa.
Kazi ya kufanya namba 6
Waulize wazazi au walezi kuhusu aina ya elimu
iliyotolewa katika jamii inayowazunguka kabla ya
ukoloni.
Elimu kabla ya ukoloni ilitolewa kulingana na shughuli za jamii
na mazingira yaliyoizunguka. Vijana na watoto walifundishwa
maarifa na stadi kama vile kilimo, uvuvi, uhunzi, ususi, upishi,
ufugaji na kadhalika. Elimu hii ilikuwa na shabaha ya kuwaandaa
watoto na vijana kwa maisha halisi katika jamii zao. Hivyo,
25
06/11/2024 11:29:36
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 25 06/11/2024 11:29:36