Page 29 - Historiayatznamaadili
P. 29
Sura ya Maendeleo ya jamii
Pili kabla ya ukoloni
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Maendeleo ni jambo muhimu katika maisha ya jamii. Katika sura hii,
utajifunza kuhusu maendeleo ya jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni.
Utajifunza kuhusu maendeleo ya jamii katika elimu, afya na makazi.
Umahiri utakaoupata, utakusaidia kutambua maendeleo ya jamii za
Kitanzania kabla ya ukoloni. Hivyo, kuthamini na kuendeleza maendeleo
hayo katika jamii zetu kwa sasa.
Fikiri
Maendeleo ya jamii nchini kabla ya ukoloni.
Dhana ya maendeleo
Kazi ya kufanya namba 1
Soma vyanzo mbalimbali, ikiwamo maktaba
mtandao kuhusu maana ya neno “maendeleo”.
Maendeleo ni hali ya ongezeko au kupiga hatua fulani. Pia,
maendeleo huhusisha ukuaji. Ukuaji huo unaweza kuwa ni
kutoka hatua moja ya chini kwenda nyingine. Kielelezo namba 1,
kinaonesha mtoto anapanda ngazi kutoka hatua ya chini kwenda
ya juu, na kila apandapo anaongeza hatua.
22
06/11/2024 11:29:35
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 22 06/11/2024 11:29:35