Page 26 - Historiayatznamaadili
P. 26
kutambua haki zao kama watoto. Kimsingi, hii humsaidia
mtoto kujilinda na ukatili, unyanyasaji na udhalilishaji dhidi
ya watoto.
(b) Kujitambua na kuchukua hatua stahiki za usalama;
FOR ONLINE READING ONLY
Mtoto anayefahamu haki zake, huweza kujitetea katika
mazingira yanayomzunguka. Pia, huweza kujisimamia dhidi
ya vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji na ukatili katika
jamii. Aidha, mtoto anayetekeleza wajibu wake, huweza
kuishi maisha salama na kupata fursa mbalimbali katika
jamii na Taifa.
(c) Kujenga uhusiano katika jamii na Taifa; Mtoto anayejua
haki zake na kutekeleza wajibu wake, ni rahisi kujenga
uhusiano mwema na kushirikiana na watu wengine katika
jamii na Taifa. Kwa mfano, mtoto anayejua haki ni rahisi
kushiriki katika mijadala ya kijamii na kisiasa kuhusu
masuala yanayohusu watoto. Hivyo, humwezesha kujenga
uhusiano na watu wengine katika jamii na Taifa.
(d) Kuwa raia mwema; Mtoto anayefahamu haki zake na
wajibu wake, ni rahisi kuwa raia mwema katika jamii na
Taifa. Utekelezaji wa haki na wajibu wa mtoto katika jamii
na Taifa, huwezesha watoto kujitambua na kuishi katika
misingi ya maadili, haki na usawa katika jamii.
(e) Kujenga maadili; Kujua haki zake, humsaidia mtoto
kutenda vitendo vyenye maadili. Pia, humwezesha kufanya
uamuzi wenye maadili kuhusu tabia zake na kutambua
jinsi ya kuwatendea mema watu wengine.
(f) Kuimarisha ustawi wake katika jamii na Taifa; Mtoto
kufahamu haki zake na kutekeleza wajibu wake, huimarisha
ustawi wake kijamii na kitaifa. Haki na wajibu wa mtoto
huongeza ushiriki wa mtoto katika shughuli za kijamii na
Taifa. Hivyo, humwezesha kuimarisha usalama na ulinzi
wa mtoto.
19
06/11/2024 11:29:34
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 19 06/11/2024 11:29:34
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 19