Page 23 - Historiayatznamaadili
P. 23
Kuwaheshimu viongozi wa serikali
Mtoto ana wajibu wa kuwaheshimu viongozi wa serikali katika
ngazi zote za uongozi. Hii ni kuanzia ngazi za Mtaa/Kijiji, Kata,
Wilaya, Mkoa na Taifa. Mtoto ana wajibu wa kuwaheshimu,
FOR ONLINE READING ONLY
kushirikiana nao na kuwatii katika matendo yaliyo mema ili
kuwezesha utekelezaji wa kazi za ustawi wa jamii na Taifa zima.
Heshima kwa viongozi, humsaidia mtoto kupata msaada na
haki zake.
Zoezi namba 3
1. Eleza umuhimu wa mtoto kuheshimu na kushirikiana na
viongozi wa serikali katika matendo yaliyo mema.
2. Orodhesha matendo yanayoashiria mtoto kujilinda na
kujijali.
Kupinga vitendo dhidi ya rushwa
Mtoto anao wajibu wa kupinga vitendo vya rushwa kwani
vinadhoofisha maendeleo ya jamii na Taifa. Vitendo vya rushwa
huwanyima watu kupata haki na huduma bora katika jamii na
Taifa. Pia, husababisha ufujaji na ubadhilifu wa rasilimali za
umma. Hivyo, mtoto ana wajibu wa kupinga vitendo vya rushwa
na kushiriki kwa vitendo kulinda rasilimali za umma. Hii ni pamoja
na kutoa taarifa za matumizi mabaya ya rasilimali za umma na
kutumia vizuri miradi ya maendeleo kama vile miundombinu
ya reli, barabara, majengo ya shule, miradi ya maji, visima,
mabomba na vinginevyo katika jamii inayomzunguka. Pia, wajibu
huu, unaweza kutekelezwa kwa kutoa elimu ya namna ya kuzuia
na kupambana na rushwa na madhara ya rushwa. Mfano, kutoa
elimu kupitia nyimbo, ngonjera, vipindi maalumu katika redio,
runinga na matamasha ya kitaifa. Vilevile, mtoto ana wajibu wa
kutoa taarifa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) akigundua vitendo vya rushwa katika jamii yake.
Kielelezo namba 7, kinaonesha watoto wenye mabango ya
kupinga vitendo vya rushwa.
16
06/11/2024 11:29:34
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 16
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 16 06/11/2024 11:29:34