Page 20 - Historiayatznamaadili
P. 20
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 6: Watoto wakishiriki kikao cha maendeleo ya jamii
Kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru na umoja wa kitaifa
Umoja wa kitaifa ndiyo nguzo ya mshikamano wa kindugu baina
ya wanajamii. Umoja huu hutafsiriwa katika namna ambayo watu
huungana na kushirikiana katika mambo ya kiitikadi, kiimani
na kiutamaduni. Watu wenye kukubaliana katika itikadi, imani
na utamaduni ni rahisi kuwa na umoja kijamii na kitaifa. Umoja
wa kitaifa huweka mazingira salama ya watu kuhusiana na
kushirikiana katika kazi ambazo ndiyo msingi wa maendeleo
ya jamii na Taifa. Ukosefu wa umoja wa kitaifa, huondoa amani
na huleta ugomvi, migogoro na mpasuko. Hivyo, ni wajibu wa
watoto kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru na umoja wa
kitaifa na katika jamii inayomzunguka.
13
06/11/2024 11:29:33
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 13
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 13 06/11/2024 11:29:33