Page 15 - Historiayatznamaadili
P. 15
Kimsingi, watoto wana wajibu wa kutekeleza katika jamii na
Taifa. Sheria ya mtoto na Katiba vinaeleza wajibu wa mtoto
katika familia, jamii na Taifa. Hii ni kwa sababu mtoto ni sehemu
ya jamii na Taifa. Kielelezo namba 3, kinaonesha watoto wenye
FOR ONLINE READING ONLY
mabango yenye baadhi ya wajibu wa mtoto.
Kielelezo namba 3: Wajibu wa mtoto katika jamii na Taifa
Kupenda kufanya kazi
Mtoto ana wajibu wa kufanya kazi katika jamii na Taifa kulingana
na umri na uwezo wake. Mtoto anapofanya kazi hujenga
mshikamano na jamii na Taifa lake. Pia, humfanya mtoto
kukubalika katika jamii yake. Jamii zote hukemea uvivu na
kutokupenda kufanya kazi. Hivyo, ni wajibu wa mtoto kupenda
na kufanya kazi ili kuwa na tabia zinazokubalika katika jamii
na Taifa. Kielelezo namba 4, kinaonesha watoto wakishiriki
kusafisha mazingira katika jamii.
Kazi ya kufanya namba 8
Fanya uchunguzi, kisha andika kazi ambazo mtoto
anaweza kushiriki katika jamii inayomzunguka.
8
06/11/2024 11:29:29
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 8 06/11/2024 11:29:29
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 8