Page 16 - Historiayatznamaadili
P. 16
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 4: Watoto wakishiriki kusafisha mazingira
Kutii sheria na kanuni za nchi na za jamii
Utii wa sheria na kanuni huwezesha watu kuishi kulingana
na maadili ya jamii na Taifa husika. Mtoto ana wajibu wa kutii
sheria na kanuni zilizopo katika jamii na Taifa lake. Mtoto asipotii
sheria za nchi, huweza kujikuta katika matatizo na vyombo
vinavyosimamia sheria hizo. Aidha, utii wa sheria na kanuni za
nchi ni muhimu kwa usalama wa mtoto mwenyewe.
Kazi ya kufanya namba 9
Soma matini kuhusu sheria za nchi, kisha andika
wajibu wa mtoto katika kuzitii sheria hizo.
Kutunza, kuheshimu na kulinda mali za umma na za jamii
Ibara ya 27 (1) na 27(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977, inaeleza wajibu wa kulinda mali asilia
za Taifa, mali za mamlaka ya nchi na mali zinazomilikiwa kwa
9
06/11/2024 11:29:30
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 9
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 9 06/11/2024 11:29:30