Page 11 - Historiayatznamaadili
P. 11
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 2: Watoto wakiwa darasani wakipata elimu
Serikali imeweka programu za kutoa elimu bila malipo katika
shule zinazomilikiwa na serikali nchini kote. Pia, imeimarisha
miundombinu katika shule hizo, na kutoa vifaa vya kufundishia
na kujifunzia ili kuwapatia watoto elimu kama haki yao ya msingi.
Hii inafanyika ili kuweka fursa sawa ya kupata elimu kwa kila
mtoto ambayo ni haki stahiki. Haki ya elimu huwezesha kila
mtoto kupata maarifa na ujuzi utakaomwezesha kuchangia
katika maendeleo yake, ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Kuheshimiwa, kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
Mtoto ana haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na kuthaminiwa
utu wake. Hii ni pamoja na kutohusishwa katika aina yoyote ya
udhalilishaji utakaomvunjia heshima mtoto. Haki hii ni ya msingi
ili kumpa mtoto haki ya faragha na usalama dhidi ya vitendo vya
ukatili, uonevu, unyanyasaji na udhalilishaji.
4
06/11/2024 11:29:27
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 4
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 4 06/11/2024 11:29:27