Page 10 - Historiayatznamaadili
P. 10
2019. Haki hizo zinatambuliwa kisheria na inakatazwa mtu au
mamlaka yoyote kukiuka haki hizo katika jamii na Taifa. Uwapo
wa haki hizo, unatoa nafasi kwa mtoto kulindwa dhidi ya ukiukwaji
wa haki za mtoto kunakoweza kusababisha unyanyasaji, ukatili
FOR ONLINE READING ONLY
na udhalilishaji wa mtoto. Mtoto si wa familia peke yake, bali ni
mali ya jamii na Taifa kwa ujumla, ndiyo maana haki za mtoto,
zimetafsiriwa katika ngazi ya jamii na Taifa. Kielelezo namba 1,
kinaonesha baadhi ya haki za mtoto katika jamii na Taifa.
Kielelezo namba 1: Haki za mtoto katika jamii na Taifa
Kupata elimu na kujielimisha
Familia inajukumu la msingi la kumpa mtoto elimu. Aidha, jamii
na Taifa wana wajibu wa kumwendeleza mtoto kwa kumpa elimu.
Hii ni pamoja na kumpa elimu ya mila na desturi za jamii na Taifa.
Pia, haki hii humpa mtoto nafasi ya kupata habari na elimu ya
kutosha ili aweze kujitambua na kuchangia katika maendeleo
ya jamii na Taifa. Aidha, mtoto ana wajibu wa kusoma kwa bidii
ili kupata elimu iliyokusudiwa. Kielelezo namba 2, kinaonesha
watoto wakiwa darasani wakipata elimu.
3
06/11/2024 11:29:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 3
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 3 06/11/2024 11:29:26