Page 9 - Historiayatznamaadili
P. 9
hata ambao siyo Watanzania lakini wanaishi Tanzania. Vilevile,
kuna sheria zinazofafanua wajibu wa mtu mzima na watoto.
Wajibu huo umezingatia umri, jinsi, na madaraka ili kurahisisha
utekelezaji wake kulingana na matarajio ya jamii na Taifa. Hivyo,
mtu asipotimiza wajibu fulani, anawajibishwa na kuadhibiwa kwa
FOR ONLINE READING ONLY
mujibu wa sheria zinazohusika.
Haki hutofautiana na wajibu. Haki hujumuisha matendo au
vitu vya msingi ambavyo mtu anastahili kupata na kutendewa
katika jamii inayohusika. Mtoto huzaliwa na hulelewa katika
jamii, ambayo hujumuisha familia, ukoo, kabila, Kijiji/Mtaa, Kata,
Tarafa na Taifa. Mazingira haya ni msingi wa mtoto kupata haki
zake. Aidha, kutokana na msisitizo wa haki za binadamu, haki
za mtoto zimewekwa kisheria zikieleza ni kipi ambacho mtu
mzima, jamii na Taifa hupaswa kutimiza kwa mtoto kama haki
zake. Haki hizo zinalenga kueleza namna jamii inavyopaswa
kumpa mtoto ulinzi, mahitaji muhimu na nafasi za ushiriki katika
kujenga jamii na Taifa. Kimsingi, mahitaji ya mtoto ndiyo hutafsiri
haki za mtoto kuanzia katika ngazi ya familia, jamii na Taifa.
Haki za mtoto katika jamii na Taifa
Kazi ya kufanya namba 2
Jadili haki za mtoto katika jamii na Taifa kama
zilivyotafsiriwa katika sheria ya mtoto, sura ya 13
ya mwaka 2009 na katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977.
Haki za mtoto zimetafsiriwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na
taratibu za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
mataifa mbalimbali. Kwa mfano, Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977, Sura ya Kwanza, Sehemu ya Tatu,
Ibara ya 12-24, inaeleza kuhusu haki za binadamu akiwamo
mtoto katika jamii na Taifa. Pia, haki za mtoto zimeelezwa katika
sheria ya mtoto, Sura ya 13 ya Mwaka 2009, toleo la mwaka
2
06/11/2024 11:29:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 2 06/11/2024 11:29:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 2