Page 13 - Historiayatznamaadili
P. 13
Kutokubaguliwa kwa njia yoyote
Mtoto ana haki ya kutobaguliwa kwa njia yoyote iwe kwa rangi,
jinsi, hali ya maisha, dini au hali itakayomfanya kuwa dhaifu na
duni. Mtoto ana haki ya kutambua ndugu na jamaa zake katika
FOR ONLINE READING ONLY
familia, ukoo na jamii inayohusika. Haki hii kimsingi inazuia
mtoto kubaguliwa na kutoa nafasi kwake ya kupata huduma za
kijamii na kisheria ili kumlinda dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji
katika jamii inayomzunguka.
Zoezi namba 1
1. Eleza matendo yanayoashiria kubaguliwa kwa mtoto.
2. Ainisha huduma anazostahili kupata mtoto katika jamii
na Taifa kwa ujumla.
Kupata hifadhi ya maisha katika jamii na Taifa
Mtoto ana haki ya kuishi kama mtu huru katika jamii na Taifa.
Haki hii inakataza mtoto kufungiwa ndani, kuhamishwa kwa
nguvu, au kunyang’anywa kwa nguvu uhuru wake kutoka katika
familia, jamii au Taifa lake. Aidha, mtoto anaweza kupata hifadhi
sehemu nyingine nje ya familia yake pale itakapothibitika kuwa
anateseka akiwa ndani ya familia yake.
Haki ya kujua utamaduni wa jamii na Taifa lake
Mtoto ana haki ya kujua utamaduni wa jamii na Taifa lake.
Haki hii humpa mtoto nafasi ya kufahamu lugha ya jamii yake,
vyakula, mavazi na michezo katika jamii na Taifa lake. Pia,
humpa mtoto nafasi ya kutambua miiko na imani za jamii yake.
Utambuzi wa utamaduni humpa mtoto nafasi ya kujua matendo
yanayokubalika na yasiyokubalika katika jamii na Taifa lake.
Vilevile, humpa mtoto nafasi ya kupata elimu ya malezi na
makuzi bora yanayoendana na mila na desturi za jamii na Taifa
kwa ujumla.
6
06/11/2024 11:29:28
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 6
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 6 06/11/2024 11:29:28