Page 14 - Historiayatznamaadili
P. 14
Kazi ya kufanya namba 5
Jadili umuhimu wa mtoto kutambua utamaduni
wa jamii na Taifa lake wakati huu wa usasa na
FOR ONLINE READING ONLY
utandawazi.
Haki hizi za mtoto zinapaswa kulindwa na watu wote kuanzia
katika ngazi ya familia, jamii na Taifa. Aidha, serikali kwa
kutambua hilo, imeweka maofisa wanaosimamia utekelezaji wa
haki za mtoto katika ngazi za Mitaa, Vijiji, Kata, Wilaya, Mikoa
na Taifa. Pia, vituo vya usalama, mfano polisi vina dawati la
masuala ya jinsia na ulinzi wa watoto. Dawati hili husimamia
utekelezaji wa haki za mtoto. Vilevile, ofisi za Kata na Mtaa/Kijiji
zina maofisa wanaosimamia haki za watoto. Aidha, viongozi wa
asasi za kidini husimamia utekelezaji wa haki za mtoto katika
jamii na Taifa. Walimu katika ngazi zote za elimu wana wajibu
wa kulinda na kusimamia haki za mtoto. Watu hawa wote wana
wajibu wa kusimamia ulinzi na usalama wa mtoto ili kuhakikisha
haki za mtoto zinalindwa ipasavyo. Hivyo, kuwezesha katika
ukuaji wa mtoto kiakili, kimwili, kisaikolojia, kimaono na kiroho.
Kazi ya kufanya namba 6
Jadili changamoto zinazoweza kuwakabili watoto
katika upatikanaji wa haki zao na jinsi ya kuzitatua
katika jamii inayokuzunguka.
Wajibu wa mtoto katika jamii na Taifa
Sheria ya mtoto ya mwaka 2009, toleo la mwaka 2019 imeeleza
wazi wajibu wa mtoto katika jamii na Taifa lake.
Kazi ya kufanya namba 7
Jadili wajibu wa mtoto katika jamii na Taifa kama
ilivyotafsiriwa katika sheria ya mtoto ya mwaka
2009, toleo la mwaka 2019 na Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
7
06/11/2024 11:29:28
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 7
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 7 06/11/2024 11:29:28