Page 21 - Historiayatznamaadili
P. 21
Kazi ya kufanya namba 13
Jadili namna ambavyo mtoto anaweza kulinda,
kuhifadhi na kudumisha uhuru na umoja wa Taifa.
FOR ONLINE READING ONLY
Mtoto anaweza kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru na umoja
wa jamii na Taifa kwa kuonesha upendo kwa watu wengine,
kushirikiana na kuthamini utu wa binadamu wenzake.
Kulinda usalama na amani ya jamii na Taifa
Pamoja na Taifa kuwa na vyombo vya kusimamia usalama
wa raia na mali zao, mtoto ana wajibu wa kulinda usalama na
amani ya jamii na Taifa lake. Wajibu huu humpa mtoto nafasi
ya uwajibikaji katika ulinzi na usalama wa jamii na Taifa lake.
Kazi ya kufanya namba 14
Jadili namna mtoto anavyoweza kushiriki katika
kulinda usalama na amani ya jamii na Taifa.
Mtoto ana wajibu wa kutoa taarifa kwenye ofisi za Mtaa/Kijiji au
polisi, iwapo ataona mazingira hatarishi ya uvunjaji wa sheria
na kanuni za jamii au nchi ili kulinda usalama na amani ya jamii
na Taifa lake. Pia, ni wajibu wa mtoto kutoa taarifa za vitendo
viovu kama vile wizi, ugomvi, udhalilishaji, ukatili na unyanyasaji.
Kujifunza utamaduni wa jamii na Taifa
Mtoto ana wajibu wa kujifunza mambo mema ya utamaduni
wa jamii na Taifa lake. Jamii ina mila na desturi zinazoongoza
wanajamii ili kuishi kulingana na mahitaji yao. Mila na desturi
hizi hueleza namna jamii inavyopaswa kuishi, kushirikiana na
kuhusiana. Pia, huelezea mienendo ya jamii kiimani, kielimu,
kimaadili na maarifa na ujuzi wa jamii inayohusika. Vilevile,
hueleza malezi, tabia njema na jinsi ya kujifunza. Kwa ujumla,
mila na desturi hubeba utambulisho wa jamii, ambao hutofautisha
14
06/11/2024 11:29:33
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 14
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 14 06/11/2024 11:29:33