Page 30 - Historiayatznamaadili
P. 30
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Mtoto akipanda hatua za maendeleo
Pia, maendeleo hutafsiriwa kwa kuangalia ongezeko katika idadi
kutoka idadi ndogo kwenda idadi kubwa. Mfano, tunapokuwa
shuleni, tumekuwa tukiongeza maarifa na stadi fulani siku hadi
siku. Huu ni mfano wa maendeleo katika ujifunzaji.
Viashirio vya maendeleo ya jamii
Kazi ya kufanya namba 2
Soma matini mbalimbali, ikiwamo maktaba mtandao
kuhusu viashirio vya maendeleo.
Viashirio vya maendeleo vinaweza kuonekana katika mabadiliko
yanayotokea kutoka hatua moja kwenda nyingine. Mfano,
mabadiliko katika ongezeko la vitu na mali. Pia, yanaweza kuwa
katika ujuzi na maarifa aliyonayo mtu na jinsi anavyoyatumia
katika kutatua changamoto anazokutana nazo. Maendeleo
yanaweza kuwa kwa mtu binafsi, jamii au Taifa kwa ujumla.
Maendeleo kwa mtu binafsi yapo katika mabadiliko ya ongezeko
la vitu, mali na hata maarifa na stadi katika maisha yake.
23
06/11/2024 11:29:36
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 23 06/11/2024 11:29:36