Page 37 - Historiayatznamaadili
P. 37
Zoezi namba 1
1. Bainisha mambo muhimu yaliyozingatiwa katika elimu
kabla ya ukoloni.
FOR ONLINE READING ONLY
2. Fafanua njia zilizotumika katika utoaji wa elimu kabla
ya ukoloni.
3. Bainisha tofauti zilizokuwapo katika utoaji wa elimu kabla
ya ukoloni na sasa.
Elimu ilitolewa kwa kuzingatia rika na jinsi. Kwa mfano, kulikuwa
na elimu kwa vijana wa kiume wakati wa balehe iliyojulikana
kama “Elimu ya Jando”. Pia, ilikuwapo elimu kwa vijana wa
kike iliyojulikana kama “Elimu ya Unyago”. Elimu hii ilikuwa na
manufaa sana katika jamii zetu. Vijana walifundishwa kuhusu
mabadiliko ya ukuaji katika miili yao na majukumu yao kwa jamii na
familia. Pia, walifundishwa kuhusu maadili ya jamii zao.
Maendeleo ya makazi ya jamii kabla ya ukoloni
Makazi ya jamii kabla ya ukoloni ni mahali ambapo jamii za kale
ziliishi. Jamii zetu kabla ya ukoloni zilikuwa na makazi kama
ilivyosasa.
Kazi ya kufanya namba 8
Waulize wazazi au walezi kuhusu:
1. Nyumba zilizojengwa na jamii yenu.
2. Mambo yaliyozingatiwa katika ujenzi wa makazi
ya jamii yenu.
Makazi ya jamii za kale yalitegemeana na mazingira ya eneo,
shughuli za kiuchumi, malighafi za ujenzi zilizopo na maendeleo
ya jamii inayohusika. Jiografia ya eneo, pia ilikuwa jambo muhimu
katika jamii kuamua eneo na aina ya makazi. Mambo haya
yalizingatiwa ili jamii iweze kuishi katika mazingira salama na
rafiki kwa maisha yao. Mfano, jamii nyingi zilijenga makazi katika
30
06/11/2024 11:29:40
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 30
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 30 06/11/2024 11:29:40