Page 36 - Historiayatznamaadili
P. 36
Pia, njia za masimulizi ya hadithi zilitumika kutoa mafunzo.
Watu wenye umri mkubwa hasa wazee, walifundisha vijana
na watoto maarifa na stadi za jamii inayohusika kwa njia ya
masimulizi. Hadithi zilizosimuliwa zilijaa mafundisho yenye
maadili, maarifa na ujuzi wa jamii. Hadithi hizo zilitumia maneno
FOR ONLINE READING ONLY
yenye mafumbo ili kufikirisha na kutoa mafunzo. Licha ya hadithi
kutumika kufundisha maarifa na ujuzi wa asili wa jamii, zilisaidia
watoto na vijana kujifunza utu, miiko, maadili na imani za jamii
zao. Vilevile, hadithi zilisaidia kujifunza majukumu muhimu ya
kiraia kwa mujibu wa mila na desturi za jamii inayohusika. Aidha,
hadithi zilisadia vijana kujifunza shughuli za uzalishaji mali.
Mbali na hadithi, palikuwapo na misemo, vitendawili na methali
vilivyotumiwa kusisitiza maadili na kanuni za jamii.
Baadhi ya maeneo yenye majabali na mapango makubwa
yalitumika kama sehemu za kujifunzia. Mababu zetu walichora
picha mbalimbali mapangoni ili kutoa elimu kuhusu mazingira,
wanyama na wadudu wakali. Pia, picha hizo zilieleza namna ya
kujenga jamii yenye amani, utulivu na kupenda kufanya kazi.
Baadhi ya ushahidi wa picha hizo, ni michoro ya mapangoni
iliyopo maeneo mbalimbali katika nchi yetu. Mfano, michoro
ya mapangoni iliyopo katika Kata ya Kolo, Wilaya ya Kondoa,
Mkoa wa Dodoma.
Elimu ilitolewa kwa lugha zilizotumiwa kwa mawasiliano katika
jamii inayohusika. Kwa mfano, Wagogo walijifunza kwa lugha
ya Kigogo na Wasukuma kwa lugha ya Kisukuma na kadhalika.
Hii ilisaidia kuwawezesha watoto kuelewa kwa urahisi mafunzo
yaliyotolewa. Njia hii ya utoaji wa elimu, ilisaidia jamii kufahamu
matarajio ya familia zao na shughuli za uchumi na jamii zao. Pia,
ilisaidia kufahamu maarifa na ujuzi wa asili wa jamii zao kwa
urahisi. Ingawa hapakuwa na mitihani kama ilivyo katika elimu
ya sasa, mwanafunzi alipimwa kutokana na utendaji wake katika
kazi. Pale mtoto alipoonekana kutokufikia vigezo vya ujifunzaji,
alifundishwa zaidi ili aweze kufikia vigezo vilivyohusika. Msingi
wa elimu yetu ya sasa nchini “Elimu ya Kujitegemea” imejengwa
kutokana na elimu ya kabla ya ukoloni.
29
06/11/2024 11:29:40
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 29 06/11/2024 11:29:40
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 29