Page 6 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 6
Utangulizi
Kitabu hiki cha Sanaa na Michezo kimeandikwa mahususi kwa
ajili ya mwanafunzi wa Darasa la Nne, Tanzania Bara. Kitabu hiki
FOR ONLINE READING ONLY
kimeandaliwa kulingana na Muhtasari wa somo la Sanaa na Michezo
uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mwaka 2023.
Baadhi ya maudhui ya kitabu hiki yamechukuliwa kutoka katika
kitabu cha Stadi za Kazi Darasa la Tano kilichochapishwa mwaka
2018 kwa kuzingatia muhtasari wa mwaka 2016.
Kitabu hiki kina sura saba, ambazo ni Uigizaji, Uimbaji na Ala za
muziki, Uchoraji, Ufinyanzi, Mazoezi ya viungo, Michezo ya asili na
ya kisasa, na Maonesho na maonyesho ya sanaa na mashindano ya
michezo. Kwa kujifunza maudhui ya kitabu hiki utakuza umahiri wa
kumudu misingi ya uimbaji na uigizaji, kuchora picha na kufinyanga
maumbo mbalimbali. Pia, utaweza kumudu mazoezi ya viungo,
kucheza michezo ya asili na ya kisasa na kushiriki katika maonesho
ya kazi za sanaa na mashindano ya michezo.
Maudhui ya sura hizi yamewasilishwa kwa njia ya matini, kazi za
vitendo, picha zenye mvuto, pamoja na mazoezi. Hivyo, unapaswa
kufanya mazoezi na kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki, pamoja na
kazi nyingine utakazopewa na mwalimu. Hii itakuwezesha kukuza
maarifa na stadi zinazokusudiwa.
Jifunze zaidi kupitia Maktaba Mtandao: https://ol.tie.go.tz au
ol.tie.go.tz
Taasisi ya Elimu Tanzania
v
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 5
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 5 19/10/2024 16:35