Page 11 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 11
(c) Kuiga miondoko ya mhusika unayetaka kumwigiza. Jifunze
jinsi ya kutembea kama mhusika huyo. Ili kuigiza vizuri
miondoko ya mhusika wako, chunguza sifa zake kama vile
namna ya kutembea, matumizi ya sauti, hali ya ukimya au
makelele;
FOR ONLINE READING ONLY
(d) Kutumia lugha ya mwili kuonesha hisia za mhusika kama
vile hofu, furaha, au hasira. Mfano, mhusika mwenye hofu
anaweza kujikunyata au kusogea nyuma. Vilevile, tumia
macho na uso kueleza hisia kwa mfano macho yanaweza
kuonesha umakini, uoga au upendo;
(e) Kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuvaa uhusika wa
mhusika wako hadi mwili wako uweze kuonyesha miondoko
hiyo kwa urahisi; na
(f) Kutumia vifaa, mapambo na maleba ili kuonesha vizuri tabia
za mhusika unayetaka kumwigiza. Maleba yanayowiana
na mwonekano wa mhusika yanaweza kusaidia katika
kuifanya miondoko yako ionekane halisi zaidi.
Mifano ya uigizaji wa miondoko ya viumbe hai
Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya namna ya kuigiza miondoko ya
mwili ya viumbe hai:
1. Kuigiza miondoko ya tembo. Simama ukiwa umenyoosha
mikono yako kama mkonga wa tembo, inama kwa mbele na
kisha fanya matendo mbalimbali kama anavyofanya tembo
kwa kutumia mkonga wake;
2. Kuigiza miondoko ya chura. Chuchumaa na kuruka kama chura
kutoka sehemu moja hadi nyingine;
3. Kuigiza miondoko ya twiga. Inua mikono yako juu kama shingo
ya twiga na kutembea kwa maringo kama anavyofanya twiga;
na
4. Kuigiza miondoko ya maua yanayochanua. Chuchumaa na
jikunje kama mbegu kisha anza kujifungua polepole huku
ukisimama kama ua linavyochanua.
4
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 4
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 4 19/10/2024 16:35