Page 13 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 13
2. Miondoko ya upepo. Simama wima na yumbisha mikono kulia
na kushoto kuashiria upepo unavovuma; na
3. Miondoko ya mvua. Nyoosha mikono, kisha tumia vidole na
viganja vya mikono kuchezesha ishara ya matone ya mvua
yanavyodondoka.
FOR ONLINE READING ONLY
Kazi ya kufanya namba 3
Tumia miondoko ya mwili na sauti kuigiza mienendo ya kiumbe
chochote kisichokuwa na uhai.
Umuhimu wa miondoko ya mwili katika uigizaji
Miondoko ya mwili ina umuhimu mkubwa katika uigizaji kwa sababu
inamsadia mwigizaji katika:
(a) Kuonesha hisia za ndani kama vile furaha, huzuni, hasira
au wasiwasi ambazo maneno hayawezi kuzionesha moja
kwa moja. Kwa mfano, kushika shavu kunaweza kuelezea
huzuni hata bila maneno;
(b) Kuongeza uhalisia katika uigizaji. Mwigizaji anapotumia
miondoko sahihi ya mwili, hadhira huweza kuamini na
kuelewa zaidi kile kinachoonyeshwa;
(c) Kuwasiliana na hadhira. Miondoko ya mwili hutumika pia
kuwasilisha ujumbe na hisia kwa hadhira, hasa kama
hakuna maneno yanayotamkwa; na
(d) Kuashiria matendo yajayo au kutoa dalili kwa hadhira
kuhusu kilicho karibu kutokea katika igizo. Kwa mfano,
mwigizaji akipiga hatua kurudi nyuma inaweza kuashiria
woga au kujitayarisha kwa hali fulani.
6
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 6 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 6