Page 10 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 10
(f) Kukodoa macho. Mwigizaji anapofanya miondoko ya
macho ya namna hii huonesha kushangaa, hofu, kutoamini
kitu au jambo lililotokea;
(g) Kushika kichwa kwa mikono yote miwili. Miondoko hii
inaweza kuashiria huzuni au mshituko. Inaweza kuonyesha
FOR ONLINE READING ONLY
mwigizaji aliyekata tamaa au anayepata shida kubwa; na
(h) Kuinua mabega na kushusha mikono. Mwigizaji anapofanya
miondoko hii, anaonesha kutojali, kukubali kushindwa au
kutokuwa na uhakika. Vilevile, inaweza kuashiria hali ya
mhusika kujisalimisha kwa hali fulani.
Kazi ya kufanya namba 1
Fanya mazoezi ya miondoko ya mwili kuonesha hisia za ndani
kama vile furaha, huzuni, hasira au wasiwasi.
Kutumia miondoko ya mwili kuigiza viumbe hai na visivyo hai
Miondoko ya mwili inaweza kutumika kuigiza tabia, mienendo na
hisia za viumbe mbalimbali kupitia lugha ya vitendo. Ili kuigiza
viumbe kwa kutumia miondoko ya mwili, ni vema kuzingatia hatua
zifuatazo:
(a) Kuchunguza tabia ya mhusika unayetaka kumwigiza
miondoko yake ili kuona anavyotembea, anavyokaa,
anavyokula au hata anavyojihami. Unaweza kutumia
TEHAMA kupata video au picha za mhusika unayemwigiza
ili kuchunguza kwa makini miondoko yake;
(b) Kuelewa maumbile ya mhusika unayetaka kumwigiza. Ni
muhimu kuchunguza umbile la mhusika. Kama ni mdudu,
chunguza idadi ya miguu, mabawa, na jinsi viungo hivyo
vinavyohusiana. Vilevile, ni vema kuzingatia uzito kama
mhusika ni mzito au mwepesi maana uzito huweza kuathiri
jinsi mhusika anavyotembea au kusonga;
3
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 3
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 3 19/10/2024 16:35