Page 15 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 15

Mazoezi ya kucheka au kulia. Mazoezi hayo humsaidia mwigizaji
          kuamsha na kumudu hisia kwa ufanisi. Kucheka na kulia ni hisia za
          kawaida lakini inaweza kuwa changamoto kuzionesha kwa uhalisia
          katika uigizaji. Mwigizaji anaweza kucheka au kulia kwa sauti ya
          chini au ya juu, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 1.
        FOR ONLINE READING ONLY
                            A                                       B
























            Kielelezo namba 1: A Mwigizaji akifanya mazoezi ya kulia na B Mwigizaji
                                   akifanya mazoezi ya kucheka


                     Kazi ya kufanya namba 5



            (a)  Igiza kucheka kwa sauti ya chini kisha ongeza sauti polepole
                  kufikia sauti ya juu.

            (b)  Igiza kulia kimya kimya, kisha kwa sauti ya chini na ongeza
                  sauti kufikia sauti ya juu.




             Zoezi la pili

            1.  Ni kitendo gani unaweza kufanya ili kuonesha kwamba una

               huzuni bila kusema neno lolote?
            2.  Eleza namna unavyoweza kuonesha hali ya hasira bila
               kupaza sauti katika uigizaji.




                                                  8




                                                                                          19/10/2024   16:35
   SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd   8
   SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd   8                                                    19/10/2024   16:35
   10   11   12   13   14   15   16   17   18   19   20