Page 20 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 20
(c) Kuzingatia kasi ya wimbo. Mwimbaji anapaswa kuimba kwa
kuzingatia kasi sahihi ili kuwezesha maneno kutamkwa
kwa wakati sahihi bila kuwahi au kuchelewa; na
(d) Kujua maana ya maneno. Mwimbaji anapojua maana ya
maneno, ataweza kutamka maneno kwa hisia zinazofaa,
FOR ONLINE READING ONLY
kulingana na muktadha. Hii hufanya maonyesho kuvutia
zaidi hadhira.
Kazi ya kufanya namba 1
Imba wimbo wa uzalendo ufuatao kwa kuzingatia matamshi
sahihi.
Tazama Ramani
(a) Tazama ramani utaona nchi nzuri,
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania,
Majira yetu haya yangekuwaje sasa?
Utumwa wa nchi Nyerere aliukomesha!
(b) Chemchem ya furaha ama nipe tumaini,
Kila mara kwako niwe nikiburudika,
Nakupenda hasa hata nikakufasili,
Nitalalamika kukuacha Tanzania,
Majira yetu haya yangekuwaje sasa?
Utumwa wa nchi Karume aliukomesha!
(c) Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde nami nikulinde mpaka kufa,
Majira yetu haya yangekuwaje sasa?
Utumwa wa nchi Nyerere aliukomesha!
13
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 13
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 13 19/10/2024 16:35