Page 16 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 16
Mazoezi ya kutoa sauti katika uigizaji
Sauti ni mojawapo ya nyenzo kuu katika uigizaji. Utoaji sauti ni zoezi
la kutoa na kudhibiti sauti ili kuweza kusikika vizuri kwa hadhira
kulingana na muktadha. Kutumia sauti ipasavyo ni muhimu kwa
mwigizaji, kwani huisaidia hadhira kuelewa igizo husika. Mazoezi
FOR ONLINE READING ONLY
ya utoaji sauti yanaweza kuwa ya kufurahisha na kuvutia sana.
Mazoezi ya sauti katika uigizaji hujumuisha mazoezi ya kuvuta na
kutoa pumzi na kuongea kwa umbali.
Mazoezi ya kuvuta na kutoa pumzi
Mazoezi ya kuvuta na kutoa pumzi kwa mwigizaji yanalenga
kumsaidia katika kudhibiti pumzi yake vizuri. Hii humsaidia kutoa
sauti yenye nguvu na kuimarisha uigizaji awapo jukwaani. Yapo
mazoezi mbalimbali ya kuvuta na kutoa pumzi kama vile kuvuta na
kutoa pumzi nzito na kwa kasi.
Kazi ya kufanya namba 6
Fanya mazoezi ya kuvuta na kutoa pumzi kwa kufuata hatua
zifuatazo:
(a) Simama wima huku ukiwa umeachanisha miguu kidogo;
(b) Weka mikono yako tumboni;
(c) Vuta pumzi kwa pua huku ukihisi tumbo kutanuka; na
(d) Kisha, achia pumzi polepole kupitia mdomo, ukihisi
tumbo kupungua.
Rudia hatua hizi mara tano.
Mazoezi ya kuongea kwa umbali
Mazoezi ya kuongea kwa umbali humsaidia mwigizaji kubadilisha
sauti yake kulingana na ukubwa wa jukwaa na umbali kati yake na
hadhira. Kielelezo namba 2 kinaonesha mwigizaji akifanya mazoezi
ya kuongea kwa umbali.
9
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 9 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 9