Page 19 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 19
Sura ya Pili
Sura ya Pili
Uimbaji na ala za muziki
Uimbaji na ala za muziki
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Uimbaji unaweza kuhusisha sauti ya mwanadamu pekee au
mchanganyiko wa sauti ya mwanadamu na sauti za ala za
muziki. Katika sura hii, utajifunza namna ya kuimba kwa sauti
mbili kwa kuzingatia matamshi sahihi na toni. Pia, utajifunza
uimbaji unaosindikizwa na ala za muziki. Umahiri utakaoujenga
utakuwezesha kuimba nyimbo mbalimbali kwa ustadi.
Fikiri
Uimbaji kwa sauti mbili.
Kuimba kwa kuzingatia matamshi sahihi
Kujifunza matamshi sahihi ni muhimu kwa mwimbaji bora. Mwimbaji
anapaswa kuzingatia utamkaji sahihi wa maneno ili kufikisha ujumbe
uliokusudiwa. Mambo muhimu ya kuzingatia ili kutamka maneno
kwa usahihi wakati wa uimbaji ni pamoja na:
(a) Kufungua mdomo vizuri wakati wa kuimba. Ufunguaji mzuri
wa mdomo husaidia katika utamkaji sahihi wa irabu na
konsonanti. Hivyo, mwimbaji anapaswa kutamka maneno
kwa usahihi ili kueleweka kwa wasikilizaji;
(b) Kupumua kwa usahihi wakati wa kuimba. Mwimbaji
anapaswa kuvuta hewa ndani taratibu na kwa kina na kisha
kuitoa kwa kiasi ili kudhibiti mtiririko wa hewa. Hii inasaidia
kuepuka kupungukiwa pumzi wakati wa uimbaji;
12
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 12
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 12 19/10/2024 16:35