Page 22 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 22
Kuimba kwa sauti mbili
Uimbaji unaohusisha sauti mbili hujumuisha waimbaji wawili au
makundi mawili kutoa sauti mbili tofauti kwa wakati mmoja. Sauti
hizi mbili huimbwa kwa pamoja kwa kuzingatia usawa. Uimbaji wa
sauti mbili unahitaji umakini mkubwa na ujuzi wa kutosha. Waimbaji
FOR ONLINE READING ONLY
wa sauti mbili lazima washirikiane kwa usawa. Katika hatua hii
utajifunza sauti ya pili ili kumudu uimbaji wa sauti mbili.
Sauti ya pili inachangia katika kuleta mwafaka wa sauti katika uimbaji.
Sauti ya pili inakua chini zaidi ya sauti ya kwanza. Katika uimbaji wa
sauti mbili mwimbaji anatakiwa kuzingatia matamshi sahihi na toni
wakati wa kuimba ili wimbo uwe na mvuto kwa hadhira.
Kazi ya kufanya namba 3
(a) Tembelea tukio lolote katika jamii yako linalohusisha uimbaji
au tafuta matukio yaliyorekodiwa katika vyanzo mtandao
na bainisha uimbaji wa sauti mbili;
(b) Chagua wimbo wowote na imba kwa sauti ya kwanza; kisha
(c) Imba wimbo huo huo kwa sauti ya pili.
Umuhimu wa kuimba kwa sauti mbili
Kuimba kwa sauti mbili ni sehemu muhimu ya uimbaji ambayo
inasaidia kuimarisha ujuzi wa uimbaji. Zifuatazo ni faida za kuimba
kwa sauti mbili:
(a) Kuufanya wimbo uwe na mvuto. Sauti mbili zinapounganishwa
huunda mchanganyiko wa sauti wenye ladha inayovutia zaidi.
Muunganiko wa sauti hizi unasaidia kuleta hisia tofauti kama
furaha au amani;
(b) Kujenga ujuzi wa kusikiliza. Ili kuimba kwa sauti mbili kwa
usahihi, waimbaji wanahitaji kusikiliza kwa makini sauti za
wenzao. Kusikiliza kwa makini husaidia kujenga uwezo wa
kuzingatia sauti nyingine huku waimbaji wakidumisha sauti
15
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 15
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 15 19/10/2024 16:35