Page 23 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 23
yao wenyewe. Hii ni hatua muhimu katika kujifunza uimbaji
na kuimarisha uwezo wa kusikiliza;
(c) Kuimarisha ushirikiano. Waimbaji wanapoimba kwa sauti
mbili, hujifunza umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano.
Kwa kuwa kila sauti ni muhimu katika kuleta uwiano, waimbaji
FOR ONLINE READING ONLY
wanajifunza jinsi ya kushirikiana vizuri, ambapo kila mmoja
anachangia kwa usawa katika kundi. Hii husaidia kujenga
tabia ya kufanya kazi pamoja na huwafundisha uvumilivu na
kuelewana na wenzao; na
(d) Kujenga ujasiri na kujiamini. Kufanikiwa kuimba kwa sauti
mbili huongeza kujiamini kwa waimbaji. Waimbaji wanapojua
wanaweza kuimba kwa usahihi na ushirikiano, huwa na
ujasiri wa kuimba mbele ya watu. Hii ni hatua muhimu katika
kujenga ujasiri binafsi na uwezo wa kujieleza kupitia uimbaji.
Uimbaji wa kusindikizwa na ala za muziki
Ala za muziki hutumika kusindikiza uimbaji. Sanaa hii inahitaji ujuzi
wa kiufundi. Kuna mambo muhimu ya kuzingatia katika uimbaji
unaosindikizwa na ala za muziki. Waimbaji na wapiga ala za muziki
wanapaswa:
(a) Kufanya mazoezi ya pamoja mara kwa mara;
(b) Kujipanga katika mpangilio sahihi. Kama waimbaji ni zaidi
ya wawili, namna ya kusimama inaweza kuwa nusu duara.
Mbele wanasimama wanaoimba sauti ya kwanza wakifuatiwa
na wa sauti ya pili. Wapigaji wa ala za muziki nao hujipanga
pembeni au nyuma ya waimbaji kutegemeana na aina na
idadi ya ala wanazopiga;
(c) Kutambua vipengele vya muziki vinavyohusika. Hatua hii ni
muhimu kwa mwimbaji kuimba kama ilivyokusudiwa; na
(d) Kuzingatia uwiano wa sauti za waimbaji na za ala za muziki.
16
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 16 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 16