Page 24 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 24
Namna ya kujipanga waimbaji na wapiga ala za muziki
Waimbaji na wapiga ala za muziki wana namna mbalimbali za
kujipanga jukwaani. Wanaweza kujipanga jukwaani kulingana na
idadi ya sauti zinazoimbwa na aina na idadi ya ala zinazotumika.
Lengo ni kupata ubora na uwiano wa sauti za waimbaji na zile
FOR ONLINE READING ONLY
zinazotolewa na ala za muziki. Ili kuwa na mpangilio mzuri, mambo
yafuatayo yanaweza kuzingatiwa:
(a) Waimbaji wa sauti ya kwanza wanapaswa kuwa pamoja;
(b) Waimbaji wa sauti ya pili wanapaswa kuwa pamoja;
(c) Wapigaji wa ala za aina moja wanapaswa kuwa pamoja; na
(d) Wapigaji wa ala za muziki zenye sauti ya chini wasiwe karibu
na wapigaji wa ala zenye sauti ya juu, kama inavyoonekana
katika Kielelezo namba 1. Hii ni kwa sababu ukichanganya
ala zenye sauti ya chini na zenye sauti ya juu, zile zenye
sauti ya chini hazitasikika vizuri.
Kielelezo Na 1: Wanafunzi wakiimba huku wakisindikizwa na ala
za muziki
17
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 17
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 17 19/10/2024 16:35