Page 29 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 29
Hatua za kuchora picha njiti ya umbo la binadamu
(i) Fikiria uelekeo wa umbo la binadamu. Chagua upande
umbo litaelekea kama ni kulia au kushoto;
(ii) Chora duara la kichwa. Anza na duara dogo juu ya
FOR ONLINE READING ONLY
karatasi yako. Hili litakuwa kichwa cha picha njiti ya
umbo la binadamu;
(iii) Chora shingo na mabega. Chora mstari wa msalaba
unaoungana na kichwa;
(iv) Chora kiwiliwili (kifua na tumbo). Chora mstari wima
moja kwa moja kutoka kichwani. Mstari huu utakuwa
umbile la kiwiliwili la picha njiti ya umbo la binadamu;
(v) Chora mikono. Chora mistari miwili inayotoka sehemu
ya juu ya mstari wa kiwiliwili. Mistari hii inawakilisha
mikono. Unaweza kuongeza miduara midogo mwishoni
kwa ajili ya viganja;
(vi) Chora miguu. Chora mistari miwili inayotoka chini
ya mstari wa msalaba. Mistari hii inaonesha miguu.
Unaweza kuongeza miduara midogo mwishoni kwa ajili
ya kuonesha nyayo za miguu;
(vii) Koleza mistari. Koleza mistari ya picha yako kwa kutumia
penseli, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba
2.
22
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 22 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 22