Page 33 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 33
(iii) Chora mistari ya msingi. Tumia mistari ya msingi kuunda
umbo la kitu unachochora. Kwa mfano, kama unachora
uso, anza na mduara wa kichwa na mistari ya usawa na
wima kwa ajili ya macho, pua na mdomo;
(iv) Ongeza maelezo. Polepole ongeza maelezo zaidi kwa
FOR ONLINE READING ONLY
kutumia mistari. Hii inaweza kujumuisha mistari ya
nywele, mavazi au maumbo mengine;
(v) Weka kivuli. Weka kivuli ili kuonesha kina na uhalisia
kwenye mchoro wako. Unaweza kutumia pamba
kusambaza na kuchanganya mistari na kuunda kivuli
laini; na
(vi) Rekebisha na kumalizia. Angalia mchoro wako kwa
makini na rekebisha sehemu yoyote inayohitaji
marekebisho ikiwa ni pamoja na kufuta alama zisizo
hitajika.
Kazi ya kufanya namba 3
(a) Chora mchoro wa dawati, meza, na kiti bila kuinua penseli
yako kutoka kwenye karatasi. Zingatia pembe na maumbo
ya kitu unachochora; na
(b) Onesha michoro hiyo darasani kwa ajili ya majadiliano.
Kazi ya kufanya namba 4
(a) Tumia penseli kuchora maumbo rahisi kama duara, mraba
na pembetatu kwenye karatasi.
(b) Onesha michoro hiyo darasani kwenu kwa ajili ya
majadiliano.
26
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 26
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 26 19/10/2024 16:35