Page 35 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 35
Sura ya Nne
Sura ya Nne
Ufinyanzi
Ufinyanzi
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Udongo wa mfinyanzi una matumizi mbalimbali katika jamii nyingi
za Kitanzania. Katika sura hii, utajifunza kufinyanga kwa njia ya
bapa na pindi. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kufinyanga
vifani na mapambo mbalimbali.
Fikiri
Njia mbalimbali za kufinyanga.
Kufinyanga kwa njia ya bapa
Njia hii inafaa kutumika kufinyanga vitu vyenye maumbo ya ukumbi
kama vile maumbo ya mchemraba, mchemstatili, mcheduara na
piramidi; kama yanavyoonekana katika Kielelezo namba 1.
Kielelezo namba 1: Maumbo yaliyofinyangwa kwa njia ya bapa
Vifaa vya ufinyanzi
Sanaa ya ufinyanzi huhitaji vifaa vifuatavyo:
(i) Udongo wa mfinyanzi;
(ii) Maji;
28
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 28
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 28 19/10/2024 16:35