Page 38 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 38
Kazi ya kufanya namba 1
(a) Finyanga angalau vifani viwili kwa kutumia njia ya bapa;
(b) Onesha darasani kwa ajili ya majadiliano, kisha;
(c) Tunza vizuri vifani ulivyofinyanga kwa ajili ya maonesho ya
FOR ONLINE READING ONLY
sanaa shuleni.
Kufinyanga kwa njia ya pindi
Njia hii inafaa kwa kufinyanga vifani vyenye maumbo ya vimo
virefu kama vile mitungi na vyungu virefu vya maua, kama
vinavyoonekana katika Kielelezo namba 6.
Kielelezo Namba 6: Vifani vilivyofinyangwa kwa njia ya pindi
Hatua za kufinyanga kwa njia ya pindi
(a) Chagua kifani unachotaka kufinyanga;
(b) Sukuma udongo mpaka uwe bapa, kama inavyoonekana
katika Kielelezo namba 7;
(c) Kata udongo uliosukuma ili kupata kitako cha sura
unayopenda;
31
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 31
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 31 19/10/2024 16:35