Page 42 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 42
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo Namba 13: Kifani kilichoachwa wazi ili kipungue maji
(l) Endapo unapumzika kwa muda mrefu, funika kifani
kwa karatasi ya mfuko wa nailoni au plastiki ili kisikauke
kabla hakijakamilika;
(m) Wakati unalainisha unamu wa ukuta, usitumie maji
mengi kwani yatalainisha kifani na kuwa dhaifu;
(n) Sawazisha kuta za nje na ndani ya kifani kwa kutumia
kitu bapa kama vile kipande cha kioo au mfuko wa
plastiki. Pia, unaweza kusawazisha sehemu ya ndani tu
na kuacha sehemu ya nje ikabaki kama ilivyo; na
(o) Weka nakshi kabla chombo hakijakauka kabisa,
kisha anika chombo kivulini ili kikauke taratibu, kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 14.
35
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 35 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 35