Page 47 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 47
Hatua za kufanya:
1. Panga koni katika muundo wa duara kwenye eneo wazi zikiwa
katika umbali wa hatua 3 hadi 5 kutoka koni moja kwenda
nyingine, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 1;
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo Na 1: Koni sita zilizopangwa katika umbo la duara
2. Kaa katika jozi au vikundi, huku kila kundi likianzia kwenye koni
tofauti;
3. Baada ya amri ya mwongozaji anza mzunguko kwa kufanya
zoezi moja la unyumbufu lililoteuliwa kwa kila koni; na
4. Baada ya kukamilisha koni zote, rudi mahali pa kuanzia.
Baadhi ya mazoezi ya kufanya kwa kila koni
1. Kunyoosha sehemu za nyuma za mwili:
(a) Simama kando ya koni na inama chini ili kugusa vidole
vya miguu, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba
2; na
(b) Shikilia kwa sekunde 10 hadi 15.
40
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 40 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 40