Page 52 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 52
Zoezi la kwanza
1. Je, zoezi la koni mzunguko lina umuhimu gani kwako?
2. Zoezi ulilofanya litakusaidia kucheza michezo gani?
FOR ONLINE READING ONLY
Kuweka puto hewani
Hili ni zoezi linalowataka washiriki kurusha puto hewani na kulizuia
lisidondoke kwa kutumia viungo mbalimbali vya mwili. Viungo
vya mwili kama kichwa, mabega, kifua, mikono, magoti na miguu
vinaweza kutumika katika kulifanya puto libaki hewani. Zoezi hili
linasaidia kuimarisha uratibu wa mwili.
Vifaa:
1. Maputo; na
2. Koni.
Jinsi ya kufanya:
1. Andaa mwili kwa kukimbia taratibu na kunyoosha miguu,
mabega na kiuno;
2. Katika eneo la wazi, andaa mipaka ya eneo la kuchezea;
3. Puliza hewa ndani ya puto;
4. Shika puto lako lenye hewa na ingia sehemu ya kuchezea;
5. Rusha juu na zuia puto lisianguke kwa kutumia mikono, kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 8, miguu, kichwa, kifua
na magoti;
45
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 45
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 45 19/10/2024 16:35