Page 56 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 56
Sura ya Sita
Sura ya Sita
Michezo ya asili na ya kisasa
FOR ONLINE READING ONLY
Michezo ya asili na ya kisasa
Utangulizi
Ipo michezo mbalimbali ya asili pamoja na ya kisasa. Katika sura
hii, utajifunza kucheza baadhi ya michezo ya asili na ya kisasa.
Umahiri utakaoujenga utakusaidia kucheza kwa ustadi michezo
ya asili na ya kisasa utakayojifunza.
Fikiri
Michezo mbalimbali ya asili na kisasa.
Michezo ya asili
Michezo ya asili ni michezo ambayo ni sehemu muhimu ya
utamaduni na urithi wa jamii zetu. Ipo michezo mingi ya asili, lakini
katika sehemu hii utajifunza kucheza michezo ya mbio za magunia
na kukimbiza kuku.
Mbio za magunia
Ni mchezo wa asili ambao washiriki hushindana kukimbia kwa kuruka
kwenda mbele wakiwa ndani ya magunia. Ni mchezo unaowataka
wachezaji kugundua mbinu itakayowawezesha kukimbia kwa kasi
na kwa urahisi huku wakiwa ndani ya gunia. Washiriki katika mchezo
huu wanaweza kuwa ni mtu mmoja mmoja au vikundi. Mara nyingi
mchezo huu hufanyika katika hafla za shule na sherehe za jumuiya.
49
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 49
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 49 19/10/2024 16:35