Page 58 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 58
Kazi ya kufanya namba 1
Fanya mazoezi ya mchezo wa mbio za magunia
Umuhimu wa mchezo wa mbio za magunia
FOR ONLINE READING ONLY
Mchezo huu una faida kwa wachezaji kama vile:
(a) Kuburudisha washiriki na watazamaji;
(b) Kujenga urafiki na ushirikiano;
(c) Kuongeza uwezo wa kufikiri;
(d) Kuchangamsha miili ya washiriki;
(e) Kukuza ari ya ushindani;
(f) Kujenga na kuimarisha afya za wachezaji; na
(g) Kuibua vipaji vya kukimbia.
Zoezi la kwanza
1. Je, umejisikiaje ulipocheza mchezo wa mbio za magunia?
2. Je, ulipata changamoto gani wakati wa kucheza mchezo
huu?
3. Je, ni mbinu gani uliitumia kucheza mchezo huu bila
kuanguka?
Mchezo wa kukimbiza kuku
Mchezo huu ni wa asili na ni maarufu sana kwenye baadhi ya maeneo;
hasa kwenye mabonanza ya watoto au matamasha ya michezo.
Ni mchezo unaoweza kuchezwa na watu wa rika zote. Lengo la
mchezo huu ni kufurahisha, kuimarisha afya ya mwili na kujenga
ushirikiano miongoni mwa wachezaji. Ni muhimu kuhakikisha kuwa
kuku atakayetumika hatadhurika wala kuumizwa wakati wa kucheza
mchezo huu.
51
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 51
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 51 19/10/2024 16:35