Page 61 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 61
Michezo ya kisasa
Michezo ya kisasa ni michezo ambayo asili yake siyo katika jamii
zetu za Kitanzania. Michezo hii ilianza kuchezwa katika maeneo
mengine kama vile Bara la Asia na Ulaya. Michezo ya kisasa ina
umaarufu mkubwa duniani. Ipo michezo mingi ya kisasa. Baadhi ya
FOR ONLINE READING ONLY
michezo hiyo ni sarakasi, mpira wa miguu na netiboli.
Mchezo wa sarakasi
Mchezo wa sarakasi ni aina ya mchezo au shughuli ambayo
inajumuisha kuonesha ustadi wa kimwili, ujasiri na mazoezi
mbalimbali ambayo yanafanyika mbele ya watazamaji. Katika
sarakasi, washiriki wanaweza kufanya hatua mbalimbali za
kufurahisha au za kustaajabisha kama vile kuruka, kujisawazisha,
kucheza na vifaa mbalimbali na kuunda maumbo mbalimbali
ardhini na hewani. Mchezo wa sarakasi hufanywa ili kutoa burudani
kwa watazamaji. Ifuatayo ni baadhi ya michezo inayohusika katika
sarakasi:
Mwendo wa kaa
Hapa mchezaji atatakiwa kutembea kwa mikono na miguu kama
atembeavyo mnyama kaa.
Jinsi ya kucheza:
1. Andaa mwili kwa kukimbia taratibu kwa dakika 2 hadi 3 na
kujinyoosha mwili;
2. Lala chali ukiwa umekunja miguu, na mikono ikiwa chini mbele
ya kichwa, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 3;
54
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 54 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 54