Page 59 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 59
Namna ya kucheza:
1. Andaa kuku mwenye afya njema. Anaweza kuwa jogoo au
koo;
2. Kaeni katika timu mbili. Kila timu iwe na wachezaji wasiozidi
wanne kutegemea ukubwa wa kiwanja;
FOR ONLINE READING ONLY
3. Wanafunzi wasiocheza watengeneze duara ili kuzuia kuku
asitoke anapokimbizwa;
4. Mwongozaji ataanzisha mchezo kwa kumtupia kuku katikati
ya mduara, kisha kupuliza kipenga kuanzisha mchezo; na
5. Baada ya amri ya mwongozaji, kimbiza kuku uweze
kumkamata, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 2.
Kielelezo 2: Wanafunzi wakishindana kumkimbiza kuku
Mambo ya kuzingatia
Kama ilivyo kwa michezo mingine, katika mchezo wa kukimbiza
kuku ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:
(a) Mchezo huu huchezwa na wavulana na wasichana.
Wasichana hushindana wenyewe na wavulana vivyo hivyo;
52
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 52
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 52 19/10/2024 16:35