Page 57 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 57
Namna ya kucheza:
1. Fanya mazoezi ya kuandaa mwili kwa kukimbia polepole kwa
dakika 2 hadi 3;
2. Weka alama ya kuanzia na kumalizia kwenye eneo la kuchezea.
FOR ONLINE READING ONLY
Umbali unaweza kuwa kati ya mita 25, 50, 75 au 100 kutegemea
na uwezo wa wachezaji;
3. Vua viatu, na chukua gunia lako la kukimbilia;
4. Simama kwenye mstari wa kuanzia mbio;
5. Ingiza miguu kwenye gunia na hakikisha linavuka kiuno;
6. Shikilia gunia kwa mikono lisidondoke;
7. Subiri amri ya mwongozaji;
8. Baada ya amri ya mwongozaji anza kukimbia kwa kuruka kwa
miguu miwili kwa pamoja kwenda mbele;
9. Kimbia kwa kasi kuelekea mstari wa kumalizia, kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 1; na
10. Mshindi ni yule atakayekuwa wa kwanza kuvuka mstari wa
kumalizia.
Kielelezo 1: Wanafunzi wakishindana katika mchezo wa mbio za magunia
50
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 50
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 50 19/10/2024 16:35