Page 63 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 63
Kutembea kwa mikono
Hapa mchezaji atatakiwa kutembea kwa mikono kama vile
utembeavyo kwa miguu. Katika kutembea kwa mikono unatakiwa
kujitahidi kulinda msawazo wa mwili ili kuepuka kuanguka.
FOR ONLINE READING ONLY
Jinsi ya kucheza:
1. Andaa mwili kwa kukimbia taratibu kwa dakika 2 hadi 3 na
kujinyoosha mwili;
2. Simama kwa mikono kwa usaidizi wa mwenzio au ukuta, kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 5;
Kielelezo Na 5: Mwanafunzi akisimama kwa mikono kwa usaidizi
wa mwenzake
3. Weka mwili katika hali ya msawazo mzuri kuepuka kuanguka,
kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 6;
4. Angalia mbele kabla ya kuanza kutembea;
56
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 56
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 56 19/10/2024 16:35