Page 68 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 68
Sura ya Saba
Sura ya Saba
Maonesho na maonyesho ya sanaa na mashindano ya michezo
Maonesho na maonyesho ya sanaa na
FOR ONLINE READING ONLY
mashindano ya michezo
Utangulizi
Katika sura zilizotangulia umejifunza uigizaji, uimbaji na ala
za muziki, uchoraji na ufinyanzi. Vilevile, umejifunza kuhusu
mazoezi ya viungo na michezo ya asili na ya kisasa. Katika sura
hii, utajifunza namna ya kufanya maandalizi na kushiriki katika
maonesho na maonyesho ya sanaa na mashindano ya michezo
kwa ngazi ya shule. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha
kushiriki katika maonesho na maonyesho mbalimbali ya sanaa
na mashindano ya michezo shuleni na kwenye jamii.
Fikiri
Namna ya kushiriki maonesho na maonyesho ya sanaa, na
mashindano ya michezo katika ngazi ya shule
Maonesho na maonyesho ya sanaa na mashindano ya michezo
Maonesho na maonyesho ya sanaa pamoja na mashindano
ya michezo shuleni ni njia nzuri ya kuibua na kuendeleza vipaji
mbalimbali. Unapopata fursa ya kushiriki kuonesha na kuonyesha
kazi mbalimbali za sanaa na kufanya mashindano ya michezo kwa
ngazi ya shule utaweza kuimarisha kipaji chako na kuwa mahiri
katika fani hizo. Maonesho ya sanaa yatahusisha uchoraji na
ufinyanzi, wakati maonyesho ya Sanaa za jukwaani yatahusisha
uigizaji na uimbaji. Mashindano ya michezo yatajumuisha mazoezi
ya viungo na michezo ya asili na ya kisasa.
61
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 61
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 61 19/10/2024 16:35