Page 70 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 70
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo Namba 1: Waigizaji wakifanya onyesho jukwaani
Kazi ya kufanya namba 1
Fanya mchezo wa kuigiza wa dakika 10 hadi 15 wenye ujumbe
kwa jamii.
Maonesho ya sanaa sanifu
Katika ngazi ya shule, maonesho haya yanahusisha kuonesha
kazi za ubunifu wa sanaa sanifu zilizofanywa kwa kipindi fulani,
kwa mfano kuanzia mwezi hadi mwaka kutegemeana na onesho
lenyewe. Onesho litahusisha kuona vitu mbalimbali vilivyotokana na
uchoraji na ufinyanzi. Ili kushiriki katika maonesho ya sanaa sanifu
kwa ngazi ya shule ni vyema kuzingatia hatua zifuatazo:
1. Chagua jina la onesho litakaloendana na kazi za sanaa sanifu;
ni vyema kuchagua jina ambalo linagusa maisha kwenye jamii
unayotoka.
63
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 63
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 63 19/10/2024 16:35