Page 74 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 74
wimbo unaoupenda na wenye ujumbe na mvuto ambao
unagusa maisha ya watu kwenye jamii unayotoka;
3. Tenga muda wa kutosha wa kufanya mazoezi. Mazoezi haya
yahusishe mazoezi ya sauti, uimbaji na matumizi ya ala za
FOR ONLINE READING ONLY
muziki ulizojifunza. Kama ni wimbo utakaoimbwa na kikundi,
kaa na wenzako ili kufanya maandalizi kwa pamoja. Maandalizi
mazuri yanamfanya mwimbaji awe na ujasiri na hivyo kufanya
vizuri mbele ya hadhira;
4. Kabla ya onyesho, fika katika eneo au jukwaa litakalotumika na
kufanya ujaribishaji wa muda mfupi wa namna utakavyoimba
siku ya onyesho. Ujaribishaji huu ni pamoja na kulifahamu
jukwaa na kujaribisha utendaji kazi wa ala za muziki
zitakazotumika;
5. Siku ya onyesho, tenga muda wa kutosha wa kupumzika kabla
ya muda wa onyesho. Hakikisha unafika mapema katika eneo
ambapo onyesho litafanyika;
6. Jiamini na maandalizi uliyoyafanya na epuka kuonyesha dalili
za kutaka upendeleo unaoweza kukuingiza kwenye vitendo
vya rushwa; na
7. Wakati wa onyesho la uimbaji, wasilisha hisia kwa usahihi.
Kama ni tukio la furaha onesha uso wa tabasamu na raha;
na ikiwa ni tukio la huzuni onesha uso wa kusikitika au kukata
tamaa. Hisia hizo zioneshwe kwa sauti na matendo.
67
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 67
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 67 19/10/2024 16:35