Page 71 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 71
2. Fanya maandalizi na wenzako ili kuibua mbinu bora za
kutayarisha onesho na uwasilishaji wenye mvuto.
3. Tayarisha ratiba fupi ya maandalizi itakayoonesha utafutaji
wa eneo la maonesho, kama vile uwanjani au chini ya mti;
utambuzi na utayarishaji wa kazi za sanaa zitakazooneshwa;
FOR ONLINE READING ONLY
mpangilio na uwekaji wa kazi za sanaa ndani ya eneo la
maonesho; muda na tarehe ya kufanyika kwa onesho.
4. Tayarisha vifaa vitakavyotumika kuandaa eneo la onesho.
Baadhi ya vifaa hivyo ni:
(a) Misumari midogo;
(b) Kitambaa kikubwa;
(c) Gundi;
(d) Meza na viti;
(e) Mkasi;
(f) Wembe;
(g) Karatasi ngumu;
(h) Nyundo; na
(i) Pini.
5. Tayarisha orodha ya kazi za sanaa zilizochaguliwa kuoneshwa.
(a) Chagua kazi katika uwiano mzuri. Chagua mchanganyiko
wa picha na maumbo ya kufinyanga katika uwiano mzuri
kutegemeana na ukubwa wa eneo na idadi ya wanafunzi.
(b) Weka kumbukumbu nzuri ya kazi zilizochaguliwa.
6. Tundika au weka kazi za sanaa katika eneo la kuzionesha,
kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 2.
7. Shiriki katika onesho kwa kuwaelekeza watakao tazama kazi
hizo.
8. Mwisho wa onesho kusanya kazi na safisha eneo ili libaki safi.
64
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 64
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 64 19/10/2024 16:35