Page 75 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 75
Kazi ya kufanya namba 3
(a) Andaa wimbo mfupi na wenye ujumbe kwa jamii yako;
(b) Fanya mazoezi ya kuimba wimbo huo kwa kusindikizwa na
FOR ONLINE READING ONLY
ala za muziki ulizojifunza; na
(c) Wasilisha wimbo wako mbele ya wanafunzi wenzako
shuleni.
Kushiriki katika mashindano ya michezo
Kwa ngazi ya shule, mashindano ya michezo yatahusisha mazoezi
ya viungo, michezo ya asili na michezo ya kisasa uliyojifunza.
Mashindano hayo yanaweza kuwa baina ya mtu mmoja mmoja au
vikundi. Washiriki wanaposhindana huwapa nafasi ya kuonesha
umahiri wao katika mchezo husika. Ili kushiriki vema mashindano
ya michezo unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Andaa eneo la kuchezea;
2. Hakikisha eneo la kuchezea ni safi na salama;
3. Andaa vifaa vya mchezo husika;
4. Vaa mavazi ya michezo husika;
5. Vaa raba za michezo husika;
6. Vua viatu unapofanya michezo ya sarakasi;
7. Fanya mazoezi ya kupasha mwili kabla ya kushiriki mchezo
husika;
8. Fanya mazoezi ili kuboresha kiwango cha uchezaji wa mchezo
husika;
68
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 68
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 68 19/10/2024 16:35