Page 69 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 69
Kushiriki sanaa za maonyesho
Ili kushiriki katika sanaa za maonyesho ni vema kuzingatia hatua
zifuatazo:
1. Chagua mada kwa ajili ya onyesho; ni vyema kuchagua
ujumbe ambao unagusa maisha ya kila siku kwenye jamii
FOR ONLINE READING ONLY
unayotoka. Mnaweza kushirikiana na mwalimu kuchagua
mada. Mifano ya ujumbe unaoweza kutumika ni athari za
rushwa, magonjwa, mazingira, elimu ya kodi, haki za watoto
na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar;
2. Kaa katika kikundi na wenzako ili kufanya maandalizi kwa ajili
ya mazoezi na onyesho lenyewe;
3. Andaeni ratiba ya maandalizi. Hakikisha kuwa ratiba inaonesha
muda wa matayarisho, mazoezi na onyesho lenyewe;
4. Fanyeni mazoezi ya onyesho kwa kuzingatia maelekezo
kutoka kwa mwalimu. Hakikisha mnafanya mazoezi ya
kutosha ili kuwa na onyesho zuri;
5. Andaeni vifaa vinavyohitajika kwenye onyesho. Vifaa hivi ni
pamoja na mavazi, mapambo na zana mbalimbali kulingana
na onyesho husika;
6. Zoezi la mwisho la onyesho lenu lifanyike katika eneo
litakalotumika siku ya onyesho;
7. Siku ya onyesho hakikisheni kuwa kila kitu kimeandaliwa
vizuri hasa jukwaa na zana;
8. Endapo mtatumia vifaa vya kielektroniki, vifaa hivyo vifanyiwe
majaribio mapema kuona kama viko salama na vinafanya
kazi vizuri. Hatua hii ifanyike chini ya usimamizi wa mwalimu
na hasa uunganishaji wa vifaa vya umeme;
9. Baada ya onyesho, hakikisha eneo lililotumika linabaki safi na
vifaa vyote vilivyotumika vimeondolewa;
10. Fanyeni tathmini kubaini ufanisi au mapungufu ya onyesho kwa
ajili ya kuboresha maonyesho mengine yatakayoandaliwa; na
11. Mwisho, pongezaneni kwa kazi mliyofanya.
62
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 62 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 62