Page 49 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 49
3. Kunyoosha sehemu ya nyuma ya paja:
(a) Keti chini ukinyoosha miguu na kuitanua;
(b) Kunja mguu mmoja;
(c) Inama kuelekea mguu ulioonyooshwa, kama inavyoonekana
FOR ONLINE READING ONLY
katika Kielelezo namba 4;
(d) Shikilia kwa sekunde 10 hadi 15; na
(e) Badilisha mguu na kurudia hatua hizo.
Kielelezo Na 4: Mwanafunzi akinyoosha sehemu ya nyuma ya paja
4. Kunyoosha kigimbi:
(a) Simama wima na pishanisha miguu;
(b) Egemea mbele ukikandamiza kisigino cha mguu wa
nyuma ardhini;
(c) Kamata mguu wa mbele kwa mikono, kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 5;
(d) Shikilia kwa sekunde 10 hadi 15; na
(e) Badilisha mguu na
kurudia hatua hizo.
42
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 42
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 42 19/10/2024 16:35